Mbunge Bwege ataka Bombardier mbili ziuzwe

Image result for PICHA YA MBUNGE BWEGE
Mbunge wa Kilwa Kusini(CUF),Suleiman Bungara (Bwege) amependekeza kuuzwa kwa ndege mbili aina ya Bombardier ili fedha zitakazo patikana zitumike katika changamoto ya upatikanaji wa maji nchini.

 

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo, Mei 8 Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka 2018/019.

“Serikali inatakiwa kutoa fedha za maendeleo kwasababu mnachokisema sio mnachokitenda leo mwananchi umuulize ndege na maji kipi kizuri , nyinyi wabunge kama kweli tuwaulize kununua ndege na kuwapa watu maji nini bora? alihoji.

“Miaka 57 ya CCM tunaongelea maji? serikali ya CCM amkeni kama hakuna Maji, kama hatupati maji serikali ya CCM bai bai, maji ni uhai tunawaambia kila binadamu kaumbwa na maji, nakusifu sana Waziri wa Maji nakusifu sana Katibu wa Wizara ya Maji,Mh. Kitila Mkumbo alikuwa huku huku kwetu. Nakuomba Mh. Spika tuunze ndege mbili tutatue tatizo la Maji,”

Aidha Mbunge huyo alisema kuwa wanaotaka maji waseme na wanaosema inunuliwe ndege wasimame na wanaotaka wasimame huku akisema wakirudi 2020 yeye sio Bwege.

Hata hivyo, Spika Job Ndugai amesema “Nakushukuru sana kwa mchango wako maneno mengine jamani tunaambiwa ukweli tu kwasababu hata tukimlaumu Waziri, Naibu wake, Katibu Mkuu tutakuwa tunawaone tuu, maana tukiacha mfuko wa maji serikali imetoa asilimia 11 ya mfuko wa maji kwa vyanzo vya ndani kwa Wizara hii.”

CHANZO KUTOKA:BONGO5